KITAIFA

JKT TANZANIA: TUTACHEZA KAMA FAINALI DHIDI YA YANGA

BENCHI la ufundi la JKT Tanzania limebainisha kuwa litacheza mechi zote ambazo zimebaki kama fainali ikiwa ni pamoja na mchezo wa leo dhidi ya Yanga.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Isamuhyo ambapo wenyeji watakuwa ni JKT Tanzania wenye pointi 22 wakiwa nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

George Mketo, kocha msaidizi wa JKT Tanzania amebainisha kuwa hawapo kwenye nafasi nzuri hivyo wanaamini mechi ambazo wanacheza ni ngumu na watapambana kupata pointi tatu muhimu.

“Tunatambua kwamba wapinzani wetu Yanga wametoka kucheza mechi kubwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika lakini maandalizi mazuri ambayo tumeyafanya yanatupa nguvu ya kupambana.

“Tupo kwenye nafasi ambayo sio nzuri hivyo kila mchezo kwetu utakuwa ni kama fainali kwa kuwa ili tutoke hapa tulipo ni lazima kupata matokeo mazuri,”.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 5-0 JKT Tanzania.

Miongoni mwa wachezaji walio kwenye kikosi cha JKT Tanzania ni nyota wa zamani wa Simba na Mtibwa Sugar, Said Ndemla.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button