KIMATAIFA
Madrid yathibitisha Rodrigo kuikosa El Clasico wikiendi hii

Baada ya kuumia juzi dhidi ya Borrusia Dortmund na kutolewa uwanjani kabla mchezo haujaisha, klabu ya Real Madrid imethibitisha kuwa itamkosa mshambuliaji wao Rodrigo Goes ambaye amepata jeraha nyama za paja ambazo linaweza kumuweka nje ya uwanja kwa wiki kadhaa.
Rodrigo ambaye alimuia juzi kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa Ulaya, Madrid ikishinda 5-2 imethibitika kuwa atakosa mchezo wa ligi kuu Hispania dhidi ya Barcelona utakaochezwa wikiendi hii.