Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST
    KITAIFA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    ChikaoBy ChikaoApril 5, 202602 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    KATIKA  msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ushindani hauishii kwenye ufungaji wa mabao pekee, bali umehamia pia kwenye ubunifu wa pasi za mwisho (assist), ambapo nyota kadhaa wameibuka na kuonesha uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi za mabao.

    Miongoni mwa majina yanayotajwa zaidi ni Elie Mpanzu wa Simba, Feisal Salum maarufu kama Fei Toto wa Azam FC, pamoja na Duke Abuye wa Yanga. Wachezaji hawa wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya timu zao, wakionesha ubora wa hali ya juu katika kutengeneza mabao.

    Leo, mbali na ushindani wa kusaka alama tatu katika Mzizima Derby kati ya Azam FC na Simba, macho ya mashabiki pia yataelekezwa kwenye vita ya nani ataongoza kwa assist kati ya Mpanzu na Fei Toto.

    Azam FC wanakuwa wenyeji wa Simba katika dimba la Azam Complex, Chamazi, huku kila timu ikihitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.

    Mpanzu, kiungo mshambuliaji wa Simba, ameendelea kuwa mhimili muhimu katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo. Utulivu wake akiwa na mpira pamoja na uwezo wa kuona nafasi mapema, umeifanya Simba kuwa hatari zaidi kila inaposhambulia.

    Kwa upande wa Azam FC, Fei Toto ameendelea kuthibitisha ubora wake kama mmoja wa viungo bora nchini. Uzoefu wake mkubwa unamwezesha kutawala kiungo na kuunganisha timu kwa ufanisi, huku pasi zake za mwisho zikiwa silaha muhimu kwa washambuliaji wa Azam kufunga mabao.

    Naye Duke Abuye wa Yanga amejiweka kwenye ramani ya ushindani huu kutokana na uwezo wake wa kupenyeza mipira hatari katika eneo la mwisho. Kasi yake pamoja na ubunifu vinamfanya kuwa tishio kwa mabeki wa timu pinzani kila anapokuwa uwanjani.

    Ushindani wa nyota hawa watatu umeongeza ladha ya ligi,  kila mmoja akipambana kuonesha ubora wake katika kila mechi. Mashabiki nao wamekuwa wakifuatilia kwa karibu kuona nani ataibuka kinara wa assist ifikapo mwisho wa msimu.

    Hadi sasa, wachezaji hawa wanalingana kwa idadi ya pasi za mwisho, kila mmoja akiwa na assist tano. Hata hivyo, macho yote yako kwa Mpanzu na Fei Toto katika mchezo wa leo, ambapo mmoja wao ana nafasi ya kumpiku mwenzake na kuchukua uongozi.

    Kwa mwendo huu, vita vya assist vinaonekana kuwa vikali zaidi kuliko ilivyotarajiwa, na bila shaka vitaendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wapenzi wa soka nchini.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleIBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA
    Next Article AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    Related Posts

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    April 19, 2026

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    April 19, 2026

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    April 19, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    SINGIDA BLACK STARS WAZIPIGA MKWARA SIMBA, YANGA NA AZAM FC

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.