Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » YANGA YATANGAZA VITA, PRESHA YAHAMIA ZANZIBAR
    KITAIFA

    YANGA YATANGAZA VITA, PRESHA YAHAMIA ZANZIBAR

    ChikaoBy ChikaoFebruary 14, 202602 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    KUELEKEA mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Kabylie, Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves amesema kikosi chake kipo tayari kwa mapambano makali dhidi ya wapinzani hao wanaoheshimika barani Afrika.

    Akizungumza kuelekea mchezo huo muhimu wa hatua ya makundi utakaochezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex,Pedro amesema JS Kabylie ni timu imara yenye uzoefu mkubwa, hasa katika michuano ya kimataifa.

    Amebainisha kuwa wapinzani wao wamewekeza kwa kiasi kikubwa msimu huu wakilenga kurejea katika historia yao ya mafanikio.

    Kocha huyo ameweka wazi kuwa maandalizi ya Yanga yamekamilika kwa kiwango cha kuridhisha, huku benchi la ufundi likifanya uchambuzi wa kina kuhusu ubora na mapungufu ya wapinzani wao.

    “Tunawafahamu vizuri. Tumechambua namna wanavyocheza na tumejiandaa kukabiliana nao kwa umakini mkubwa,” amesisitiza.

    Pedro aliongeza kuwa licha ya JS Kabylie tayari kutokuwa na presha ya kufuzu, bado watashuka dimbani kupigania heshima ya klabu yao.

    “Wanakuja bila presha kwa sababu tayari wameshatoka kwenye mashindano, lakini hilo linaweza kuwafanya wacheze kwa uhuru zaidi. Hivyo ni lazima tuwe makini kwa dakika zote 90,” amesema.

    Ameongeza  kuwa huu ni muda wa Yanga kuonyesha ubora wao na kupigania nafasi ya kusonga mbele, mechi hiyo kuwa ngumu, umuhimu wa nidhamu, umakini na kutumia vyema nafasi zitakazopatikana.

    Kwa sasa msimamo wa Kundi B unaongozwa na Al Ahly SC wenye pointi tisa, wakifuatiwa na AS FAR Rabat wenye pointi nane. Yanga wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi tano, huku JS Kabylie wakiburuza mkia kwa pointi tatu.

    Pedro anaamini kikosi chake kiko tayari kufanya hesabu sahihi na kupambana hadi mwisho, akitumaini kupata pointi muhimu zitakazowaweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua inayofuata ya mashindano hayo.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleMechi ya Yanga vs Kabylie CAF ni Lini? Tarehe, Saa na Mahali
    Next Article Viingilio vya Mechi ya Simba vs Stade Malien 14/02/2026

    Related Posts

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    April 19, 2026

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    April 19, 2026

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    April 19, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    SINGIDA BLACK STARS WAZIPIGA MKWARA SIMBA, YANGA NA AZAM FC

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.