Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home ยป Tanzania Yaiomba China Msaada Kukamilika Miundo Mbinu ya AFCON 2027
    KITAIFA

    Tanzania Yaiomba China Msaada Kukamilika Miundo Mbinu ya AFCON 2027

    ChikaoBy ChikaoFebruary 10, 202601 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Tanzania
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    Serikali ya Tanzania imeiomba Jamhuri ya Watu wa China kuunga mkono juhudi za Tanzania katika kuimarisha miundombinu ya kisasa ili kujiandaa vyema na uenyeji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027).

    Wito huo umetolewa hivi karibuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, James Millya, wakati wa hafla ya kusherehekea Mwaka Mpya wa China iliyofanyika katika Ubalozi wa nchi hiyo jijini Dar es Salaam.

    Millya amesisitiza kuwa maandalizi ya AFCON 2027 ni zaidi ya michezo, akiyataja mashindano hayo kama fursa ya kimkakati kwa ajili ya mabadiliko ya kiuchumi kwa kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia biashara na utalii, upanuzi wa miundombinu ukihusisha ujenzi na ukarabati wa viwanja vinavyokidhi viwango vya kimataifa na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania, nchi jirani za Afrika Mashariki na washirika wa kimataifa kama China.

    Naibu Waziri amebainisha kuwa uenyeji wa mashindano hayo unahitaji uwekezaji mkubwa katika mifumo ya usafirishaji, huduma za kijamii, na viwanja vya kisasa. China, ikiwa ni mshirika mkuu wa Tanzania katika ujenzi wa miundombinu mikubwa, inatajwa kuwa na mchango muhimu katika kufanikisha azma hiyo ya nchi za Afrika Mashariki.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleRASMI AL NASR YAMCHOMOA KIBU DENIS MSIMBAZI KWA MILIONI 776
    Next Article MO DEWJI AHOJI MAGEUZI SIMBA, GUMZO MTANDAONI

    Related Posts

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    April 19, 2026

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    April 19, 2026

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    April 19, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    SINGIDA BLACK STARS WAZIPIGA MKWARA SIMBA, YANGA NA AZAM FC

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.