Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » SIMBA WATIKISWA, YANGA WAPANGIA ROBO FAINALI
    KITAIFA

    SIMBA WATIKISWA, YANGA WAPANGIA ROBO FAINALI

    ChikaoBy ChikaoFebruary 10, 202602 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    yanga
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    UONGOZI wa klabu ya Yanga umeweka wazi msimamo wao wa kutokubali kushindwa, wakisema hawataki kutokea kile kilichotokea kwa wapinzani wao Simba,  walishindwa kufuzu kwa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

    Yanga ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa AS FAR Rabat kwenye mchezo wa ugenini uliochezwa dimbani Olymique, mji wa Rabat nchini Morocco.

    Kipigo hiki kimeachia Yanga  changamoto kubwa ya kupambana kwenye mechi yao ya mwisho ya makundi dhidi ya JS Kabylie ili kuepuka hatma ya kushindwa kufuzu kama ilivyotokea kwa Simba.

    Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, amesema kwamba kwa sasa klabu inawaona mbele tu, huku wakijua kwamba matokeo ya mchezo dhidi ya AS FAR Rabat hayawezi kubadilisha hali yao. Kamwe alisisitiza kuwa,

    “Yanga kwa sasa tunawaza kushinda mechi yetu ya mwisho visiwani Zanzibar. Sio kushinda pekee, bali tunataka kufuzu kwenda robo fainali kwa ushindi mkubwa.”

    Kamwe ameongeza kuwa Yanga wanajivunia uwezo wao na wana imani kwamba hakuna kitu kitakachowazuia kufuzu, “Tunataka kuonyesha maajabu kwa kushinda kwa kishindo na kufanya yote ili tufikie robo fainali.”

    Yanga inahitaji ushindi katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya JS Kabylie utakaochezwa Jumapili, Februari 15, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

    Lakini si ushindi pekee, Yanga inahitaji pia Far Rabat kupoteza mbele ya Al Ahly ili iweze kupata nafasi ya kusonga mbele.

    Katika kundi hili, Al Ahly anachukua nafasi ya juu akiwa na pointi tisa, AS FAR Rabat ina pointi nane na inashika nafasi ya pili, huku Yanga ikiwa na pointi tano.

    JS Kabylie inashikilia mkia ikiwa na pointi tatu. Endapo Yanga itashinda mechi yake ya mwisho, huku Far Rabat akipoteza mbele ya Al Ahly, basi Yanga itafuzu kwa robo fainali.

    Mechi hii itakuwa na umuhimu mkubwa kwa Yanga, kwani ushindi utahitaji jitihada za ziada na dhamira ya dhati, ili kuendelea kuandika historia yao katika michuano ya Afrika.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleMbwana Samatta na Simon Msuva Hali Ngumu Huko Walipo, Hawatupii Tena
    Next Article LOEMBA, CHAMA KUWA PAMOJA LIGI KUU HAITAELEWEKA

    Related Posts

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    April 8, 2026

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    April 8, 2026

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    April 7, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    MBAPPE: NITACHEZEA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.