Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » SIMBA WABAKI NJIA PANDA, TAFSIRI TOFAUTI YA KAPOMBE
    KITAIFA

    SIMBA WABAKI NJIA PANDA, TAFSIRI TOFAUTI YA KAPOMBE

    ChikaoBy ChikaoFebruary 9, 202601 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    MAHODHA wa Simba, Shomari Kapombe aibua gumzo baada ya kushindwa kuweka wazi maana halisi ya staili yake mpya ya kushangilia mabao, inayohusisha kutembea kama mzee anayesaidiwa na mkongojo, akisema ni staili atakayoendelea nayo kila anapofunga.

    Kapombe alionekana kwa mara ya kwanza akitumia staili hiyo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Esperance de Tunis, uliochezwa hivi karibuni, ambapo alishangilia kwa namna iliyowaacha wengi njia panda.

    Katika kushangilia huko, beki huyo wa kulia alionekana akishika mfano mkongojo, ishara iliyozua tafsiri tofauti miongoni mwa mashabiki, huku baadhi wakiamini ni ujumbe maalum aliokusudia kuuwasilisha.

    Akizungumza kuhusu staili hiyo, Kapombe amesema  ameamua kuitumia kama sehemu ya kujipa motisha binafsi, hasa kutokana na maneno ya kubezwa anayopata kutoka kwa baadhi ya watu.

    Nahodha huyo wa Simba aliongeza kuwa kila atakapopata nafasi ya kufunga, ataendelea kushangilia kwa staili hiyo ya kutembea kama mzee, kama njia ya kuwajibu wanaomdharau au kumuita mzee.

    “Hivi sasa nawaacha wanaoelewa maana yake waendelee kuelewa kwa njia yao, lakini hapo baadaye nitaweka wazi sababu hasa zilizonifanya nichague hii staili,” amesema  Kapombe.

    Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, staili hiyo ya Kapombe inalenga kuwapa majibu wale wanaomkosoa na kumbeza, huku akionyesha kuwa bado ana nguvu, ari na ‘damu inayochemka’ ndani ya uwanja.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleMILIONI 500 KUWAPELEKA YANGA ROBO FAINALI
    Next Article Mbwana Samatta na Simon Msuva Hali Ngumu Huko Walipo, Hawatupii Tena

    Related Posts

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    April 8, 2026

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    April 8, 2026

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    April 7, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    MBAPPE: NITACHEZEA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.