Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home ยป WAZIRI AWESO AWAKILISHA WAZIRI MKUU KATIKA KILELE CHA SIMBA DAY 2025
    KITAIFA

    WAZIRI AWESO AWAKILISHA WAZIRI MKUU KATIKA KILELE CHA SIMBA DAY 2025

    ChikaoBy ChikaoSeptember 10, 202501 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    simba
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso, amewasili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam akimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, kama Mgeni Rasmi katika kilele cha Wiki ya Simba (Simba Day 2025).

    Katika tukio hilo kubwa linaloendelea hivi sasa, Waziri Aweso ameungana na viongozi wa Simba SC pamoja na maelfu ya mashabiki waliomiminika kushuhudia burudani, utambulisho wa kikosi kipya cha msimu huu na shamrashamra zinazotambulisha heshima na hadhi ya klabu hiyo.

    Simba Day, ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka, ni sehemu ya utamaduni wa klabu hiyo kongwe barani Afrika, ikileta pamoja wapenzi wa soka na burudani huku ikitoa taswira ya mshikamano mkubwa kati ya klabu na mashabiki wake.

    Kilele cha maadhimisho ya mwaka huu kimeambatana na burudani kutoka kwa wasanii wakubwa, pamoja na matarajio makubwa ya mashabiki kuhusu kikosi kipya cha Simba kitakachoingia dimbani kwenye michuano ya ndani na kimataifa msimu wa 2025/26.

    Simba SC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleRASMI DEPAY AFIKIA REKODI YA VAN PERSIE UHOLANZI
    Next Article ALI KAMWE AMETOA AHADI HII YANGA DAY 2025

    Related Posts

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    April 19, 2026

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    April 19, 2026

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    April 19, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    SINGIDA BLACK STARS WAZIPIGA MKWARA SIMBA, YANGA NA AZAM FC

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.