Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » UKWELI WA ISHU YA YANGA KUACHANA NA KOCHA FOLZ
    KITAIFA

    UKWELI WA ISHU YA YANGA KUACHANA NA KOCHA FOLZ

    ChikaoBy ChikaoSeptember 29, 202502 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Cv ya Romain Folz Kocha Mpya wa Yanga 2025/2026
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    WAKATI tetesi zikieleza kuwa mabosi wa Yanga SC huenda wakaachana na Kocha Mkuu, Romain Folz ambaye amekiongoza kikosi hicho kutwaa taji la Ngao ya Jamii, Legend katika masuala ya michezo Tanzania Saleh Ally Jembe amehoji maswali mazito.

    Jembe amebainisha kuwa tetesi hizo haoni kama zina mashiko kutokana na sababu ambazo zinatajwa kutoeleweka kwani hakuna kitu ambacho hajakifanya kocha Folz.

    “Ikiwa utasema kwamba Yanga SC wanataka kumuacha Folz inabidi unaiambie kwa nini anaachwa kwa sasa? Ukiangalia ameongoza mechi tano na hajafungwa.

    “Mchezo wa kirafiki, mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC ambao ulikuwa na ushindani mkubwa. ukiachana na hilo kuna mchezo wa kimataifa Ligi ya Mabingwa Afrika ameshinda mechi zote mbili.

    “Kocha aliyepata ushindi wa jumla ya mabao 5-0 kimataifa unataka umfukuze kwa sababu ipi? Ina maana makocha wote ambao wamepata matokeo tofauti na Folz nao wafukuzwe? Kuna namna ambayo ipo kuhusu uchezeji naona wengi watakuwa hawajui.

    “Tangu zamani Yanga SC imekuwa na aina ya mchezo wa kutafuta ushindi yaani ni mpira wa mbio kisha wao wanatafuta matokeo leo hii useme wanacheza vibaya wamfukuze kocha sijui kama itakuwa hivyo lakini tusubiri na tuone,”.

    Yanga SC Septemba 30 2025 itakuwa na mchezo wa ligi ya NBC dhidi ya Mbeya City unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleMWAMUZI WA TANZANIA KUONGOZA MICHEZO YA KOMBE LA DUNIA
    Next Article TAKWIMU ZA KELVIN JOHN HUKO DENMARK

    Related Posts

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    April 8, 2026

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    April 8, 2026

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    April 7, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    MBAPPE: NITACHEZEA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.