Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » MAJIBU KUHUSU USHINDI WA SIMBA UGENINI KUWA NI BAHATI
    KITAIFA

    MAJIBU KUHUSU USHINDI WA SIMBA UGENINI KUWA NI BAHATI

    ChikaoBy ChikaoSeptember 21, 202502 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    simba
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    “Ni kweli, mijadala ipo—Simba haikucheza soka la kuvutia sana dhidi ya Gaborone United, lakini bado ikaibuka na ushindi. Wapo wanaoona kama ni dalili za udhaifu, lakini kuna mambo kadhaa ya kuzingatia kabla ya kutoa hukumu ya haraka.

    Kwanza, Simba walikabiliana na timu bora ambayo ilikuwa imepumzika na kujiandaa kikamilifu kwa mechi hiyo. Pili, Simba wamekusanya pointi tatu muhimu ugenini, jambo linalowapa nafasi kubwa ya kufanya marekebisho kwenye mchezo wa nyumbani. Tatu, ratiba ya safari zao ilikuwa ngumu mno—kuanzia baada ya mechi ngumu dhidi ya Yanga, kisha safari ndefu hadi Afrika Kusini, Gaborone na baadaye Francistown. Zaidi ya masaa 24 yamepotea angani na viwanja vya ndege, huku muda wa mazoezi na kupumzika ukiwa mdogo sana.

    Uchovu ni hali ya kawaida kwa wachezaji katika mazingira kama hayo, na bado Simba waliweza kupambana, kuonyesha nidhamu ya kiufundi na kupata matokeo wanayoyahitaji.

    Hii haimaanishi Simba wamemaliza kazi. Safari bado ni ndefu, nafasi ya kurekebisha ipo, na mchezo wa nyumbani ndiyo kipimo cha kweli cha ubora wao.

    Jambo la muhimu kwa Wanamsimbazi sasa si kulalamika wala kushusha morali, bali kuwaamini wachezaji wao. Hawa ni wanajeshi waliopambana katika mazingira magumu, na bado wameanza vyema kampeni ya msimu huu wa CAF Champions League.

    Safari imeanza, na mshindi huamuliwa mwisho, si mwanzo.” amesema Mchambuzi nguli wa soka nchini, Saleh Jembe kupitia ukurasa wake wa Instagram 

    Simba SC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleBARCELONA KUMNUNUA KANE KWA EURO MILIONI 50
    Next Article VILABU VYA TANZANIA VYAANZA NA MOTO MECHI ZA KIMATAIFA

    Related Posts

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    April 8, 2026

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    April 8, 2026

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    April 7, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    MBAPPE: NITACHEZEA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.