Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home ยป FADLU ATHIBITISHA KUONDOKA SIMBA, AWAAGA MASHABIKI KWA HESHIMA
    KITAIFA

    FADLU ATHIBITISHA KUONDOKA SIMBA, AWAAGA MASHABIKI KWA HESHIMA

    ChikaoBy ChikaoSeptember 22, 202501 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Fadlu
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    Baada ya kuagana rasmi na mabingwa wa kihistoria wa Tanzania, Simba SC, kocha raia wa Afrika Kusini Fadlu Davids sasa amejiunga na wakali wa Morocco, Raja Club Athletic, kama kocha mkuu.

    Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya karibu na klabu hiyo, makubaliano yote kati ya pande mbili yamekamilika, na Fadlu anarejea katika timu aliyowahi kuitumikia kama kocha msaidizi. Wakati huo, Raja walitwaa ubingwa wa Botola Pro bila kupoteza mchezo wowote msimu mzima, rekodi iliyowaweka kileleni barani Afrika.

    Kwa sasa, Davids yupo nchini Afrika Kusini na anatarajiwa kuondoka kesho kuelekea Morocco ili kuanza rasmi majukumu yake. Hatua hii inafungua ukurasa mpya wa maisha yake ya ukocha, safari ambayo safari hii anaingia kama kocha mkuu wa Raja Casablanca.

    Raja Club Athletic, moja ya vilabu vikongwe na vyenye mashabiki wengi barani Afrika, imepania kurejea katika nafasi ya juu zaidi, hasa kwenye mashindano ya CAF Champions League. Uongozi wa klabu hiyo umeahidi kumpa Fadlu na benchi lake la ufundi sapoti ya kutosha kuhakikisha ndoto hizo zinatimia.

    Kwa ujio wake, mashabiki wa Raja wanatarajia mwendelezo wa falsafa yake ya soka ya kushambulia kwa kasi na nidhamu ya kiufundi, huku wakiamini anaweza kurejea utukufu wa zamani wa klabu hiyo.

    Simba SC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleFADLU SAFARI YA KUIACHA SIMBA, RASMI IMEWADIA, KUONDOKA KESHO
    Next Article SIMBA YATANGAZA RASMI UWANJA WA MKAPA KUWA UWANJA WAO WA NYUMBANI 2025/2026

    Related Posts

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    April 12, 2026

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    April 8, 2026

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    April 8, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.