Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home ยป STARS ICHEZE UWANJANI MASHABIKI WACHEZE JUKWAAMI
    KITAIFA

    STARS ICHEZE UWANJANI MASHABIKI WACHEZE JUKWAAMI

    ChikaoBy ChikaoAugust 22, 202512 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    Achana na hiyo picha iliyoko mbele ya macho yako ambayo kuanzia jana ilivyopigwa mpaka leo imekuwa picha pendwa mtandaoni.

    Hao ni Wakuu wa Idara za Habari na Mawasiliano wa timu pendwa za Yanga SC na Simba SC. Mmoja Ali Kamwe. Mwingine ni Ahmed Ally.

    Leo usiku Taifa letu la Tanzania litakuwa na mchezo wa kutafuta nafasi ya kuingia Nusu Fainali ya Mashindano ya CHAN kwa mara ya kwanza. Mpinzani wetu ni Morocco ambao ni mabingwa mara mbili wa michuano hii.

    Tunawaheshimu Morocco, lakini hatuwaogopi. Kimsingi Amiri Jeshi Mkuu wa nchi Dr. Samia Suluhu Hassan ameshatimiza wajibu wake kwa kutoa kiasi cha Sh. Mil 200 kwa wachezaji wa Stars kwa ajili ya kuongeza morali ya mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

    Makocha wameshazungumza jana katika Mkutano na Wanahabari. Kila mmoja ameshatimiza wajibu wake. Tuliobaki na madeni ni makundi mawili. Sisi mashabiki jukwaani na wachezaji ndani ya kiwanja.

    Tumebaki sisi tu. Lakini zaidi ni sisi mashabiki ambao ni sehemu muhimu zaidi inayohitajika kujaa katika dimba la Benjamin Mkapa.

    Wingi wetu jukwaani ndio unapeleka deni kwa wachezaji kupambana kiwanjani. Mashabiki ni nyenzo muhimu ya ushindi katika usiku wa leo.

    Hivyo mashabiki wafahamu wazi wana umuhimu mkubwa wa kwenda kuyajaza majukwaa ya uwanja na kutengeneza hamasa kwa wachezaji wetu kiwanjani.

    Mashabiki wana mchango mkubwa katika jioni ya leo. Hata benchi la ufundi la Taifa Stars mara kadhaa limekuwa likizungumzia jambo la mashabiki kuja katika mechi za Stars. Jioni ya leo mashabiki ni muhimu zaidi.

    Kila mmoja akitimiza wajibu wake kama ambavyo Rais Samia ametimiza kwa wachezaji inawezekana kabisa kama Taifa tukaandika historia mpya ya soka letu tukiwa pamoja.

    Mungu Ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Taifa Stars. PAMOJA INAWEZEKANA.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleTANZANIA KWENYE VITA UWANJANI NA MOROCCO CHAN 2024
    Next Article CHALAMILA KUMZAWADIA GARI KIPA WA STARS ASIPORUHUSU GOLI LEO

    Related Posts

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    April 19, 2026

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    April 19, 2026

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    April 19, 2026
    View 1 Comment

    1 Comment

    1. Wanted on August 22, 2025 2:03 pm

      T-stars inaweza kuonesha kile ilicho nacho mbele ya morroco kikubwa nikuwa na nizamu uwanjani nakumuheshimu mpinzani.

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    SINGIDA BLACK STARS WAZIPIGA MKWARA SIMBA, YANGA NA AZAM FC

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.