Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » MESSI NDIO ALINIFANYA NIWE KOCHA BORA – MOURINHO
    KIMATAIFA

    MESSI NDIO ALINIFANYA NIWE KOCHA BORA – MOURINHO

    ChikaoBy ChikaoAugust 21, 202501 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    José Mourinho amefichua kwamba Lionel Messi alimfanya kuwa kocha bora, akikiri kwamba kukabiliana na Muargentina huyo mara kwa mara kulimsukuma kutafakari upya mbinu zake na kufikia kiwango cha juu zaidi cha soka.

    Mtaalamu huyo wa kireno, alipambana na Messi katika baadhi ya mechi kali katika maisha yake ya soka akiwa kocha wa Inter Milan na Real Madrid.

    Alipoulizwa na Sporty Net ataje mchezaji ambaye amemsaidia kukua, Mourinho alijibu: “Messi, kwa sababu kila nilipocheza dhidi yake alinilazimisha kufikiria sana.”

    Wakati akiwa Inter, kikosi cha Mourinho kiliishinda Barcelona ya Messi kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2010 na baadaye akiwa Real Madrid, alikabiliana na Messi mara kwa mara katika mechi za El Clasico.

    Akitafakari juu ya mechi hizo, Mourinho aliwahi kukiri kuwa uwepo wa Messi ulibadilisha njia yake ya kucheza mchezo.

     

    “Messi hakuwahi kuichezea timu yangu, lakini alicheza dhidi yangu na amenifanya kuwa kocha bora kwasababu nilijiandaa vizuri kumzuia,” alisema José Mourinho.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleBASII KWISHA MZUNGUKO KESHO FIKA KWA MKAPA TIKETI UTAIKUTA GETINI
    Next Article RAIS SAMIA AWAPA TAIFA STARS MILIONI 200 KABLA YA KUMENYANA NA MOROCCO

    Related Posts

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    April 17, 2026

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    April 16, 2026

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    April 7, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    SINGIDA BLACK STARS WAZIPIGA MKWARA SIMBA, YANGA NA AZAM FC

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.