Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » HUYU HAPA ATAJWA KUANDALIWA KUBEBA MIKOBA YA ZIMBWE JR SIMBA SC
    KITAIFA

    HUYU HAPA ATAJWA KUANDALIWA KUBEBA MIKOBA YA ZIMBWE JR SIMBA SC

    ChikaoBy ChikaoAugust 28, 202501 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Simba
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    WAKATI kikosi cha Simba SC kikitarajiwa kurejea Tanzania leo Agosti 28 2025 inaelezwa kuwa tayari benchi la ufundi lina jina la mrithi wa mikoba ya Mohamed Hussen Zimbwe Jr ambaye alikuwa nahodha mkuu msimu wa 2024/25.

    Zimbwe Jr kwa sasa hatakuwa ndani ya Simba SC msimu wa 2025/26 baada ya kupata changamoto mpya ndani ya Yanga SC. Inaelezwa kuwa benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids limechagua jina la Chamou Karabou kuwa nahodha.

    Chamou Karabou ni beki anatarajiwa kuwa nahodha wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids, rai awa Afrika Kusini. Msimu wa 2024/25 hakuwa chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Simba SC.

    Rekodi zinaonyesha kuwa Chamou alicheza jumla ya mechi 19 za ligi akikomba dakika 1,480 ni alitoa pasi moja ya goli ndani ya ligi kati ya mabao 69 yaliyofungwa na Simba SC baada ya mechi 30.

    Inaelezwa  Fadlu anamuandaa Chamou kuwa mrithi wa aliyekuwa beki wa kushoto wa timu hiyo msimu wa 2024/25, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ awe nahodha msimu ujao.

    Beki mkongwe wa kulia, Shomari Kapombe ambaye alikuwa nahodha namba tatu katika kikosi hicho, yeye atakuwa wa pili na siyo wa tatu kama ilivyokuwa msimu uliopita.

    Simba SC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticlePITIA MAGAZETI YA MICHEZO LEO TAREHE 28 AGOSTI 2025
    Next Article SIMBA KUTO KUCHEZA TENA KARIAKOO DABI, AHMED ALLY AELEZEA UKWELI

    Related Posts

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    April 8, 2026

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    April 8, 2026

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    April 7, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    MBAPPE: NITACHEZEA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.