Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » ARAFAT ASEMA MIKAKATI YA YANGA KWENYE KUIBAKISHA NGAO YA JAMII JANGWANI
    KITAIFA

    ARAFAT ASEMA MIKAKATI YA YANGA KWENYE KUIBAKISHA NGAO YA JAMII JANGWANI

    ChikaoBy ChikaoAugust 26, 202501 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Yanga
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    Klabu ya Yanga imeanza mikakati ya kuhakikisha inapata ushindi katika mchezo wake wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao wa jadi, Simba, unaotarajiwa kupigwa, Septemba 16, mwaka huu, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

    Makamu wa Rais, Arafat Haji, amesema kuwa mipango na mikakati ya mechi hiyo imeshaanza ambapo lengo ni kupata ushindi ili kuendelea kulihifadhi taji hilo.

    Alisema kuwa heshima ya Yanga kwa msimu wa 2025/26, itaanza kuwekwa katika mchezo huo.

    “Tuna kazi tarehe 16, jamaa walitamani ule mfumo ungeendelea, walitamani ungendelea kuchezwa kwa mfumo wa nusu fainali ili watukimbie tena, lakini wanasema Mungu si Athumani, kawaleta, siku hiyo tutaanza kuweka heshima ya Yanga kwa msimu wa 2025/26,” alisema Haji.

    Akaongeza: “Tutakwenda kuhakikisha Ngao ya Jamii inakwenda nyumbani, ibakie Jangwani kwa sababu ni kwao, hivyo ushirikiano wa Wanayanga wote ule uliooneshwa msimu uliopita uongezeke mara dufu msimu huu.”

    Yanga SC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleBOCCO NA MKUDE KUAGWA RASMI SIKU YA SIMBA DAY
    Next Article SELEMANI MWALIMU AWASILI TANZANIA KUJIUNGA RASMI NA SIMBA

    Related Posts

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    April 19, 2026

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    April 19, 2026

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    April 19, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    SINGIDA BLACK STARS WAZIPIGA MKWARA SIMBA, YANGA NA AZAM FC

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.