Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » RASMI: YANGA YAMNASA CASEMIRO WA ZANZIBAR KUTOKA MLANDEGE!
    KITAIFA

    RASMI: YANGA YAMNASA CASEMIRO WA ZANZIBAR KUTOKA MLANDEGE!

    ChikaoBy ChikaoJuly 24, 202511 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    yanga
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    Klabu ya Yanga imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu mpya baada ya kumtambulisha rasmi kiungo mkabaji wa Mlandege, Abdulnassir Mohammed Abdallah, maarufu kama “Casemiro”, kwa mkataba wa miaka mitatu.

    Usajili wa kiungo huyo mahiri ulimalizika tangu Julai 2, 2025, lakini klabu hiyo imemtambulisha rasmi leo, ikiwa ni sehemu ya mipango yao ya kusuka kikosi imara na chenye ushindani wa hali ya juu.

    Katika kumsajili, Yanga walishinda vita kali ya saini yake dhidi ya klabu kama Azam FC, JKT Tanzania na Singida Black Stars, ambazo zote zilikuwa kwenye harakati za kumchukua kiungo huyo tegemeo kutoka Zanzibar.

    Abdulnassir, anayefahamika kwa jina la utani la “Casemiro” kutokana na aina yake ya uchezaji wa kukaba kwa ufanisi, ni kipaji kipya kilichotoka visiwani Zanzibar, na anaonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kuziba nafasi ya kiungo mkabaji ndani ya kikosi cha Wananchi.

    Usajili huu unaashiria dhamira ya Yanga ya kuendelea kuwa na safu thabiti ya kiungo, huku wakijihakikishia nguvu mpya itakayowasaidia katika mashindano ya ndani na ya kimataifa.

    Yanga SC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleYANGA SC YAMALIZANA NA MASHINE YA MABAO
    Next Article MAGAZETI YA MICHEZO LEO ALHAMISI TAREHE 24-7-2025

    Related Posts

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    April 19, 2026

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    April 19, 2026

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    April 19, 2026
    View 1 Comment

    1 Comment

    1. Pingback: MAGAZETI YA MICHEZO LEO ALHAMISI TAREHE 24-7-2025 - SOKALEO

    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    SINGIDA BLACK STARS WAZIPIGA MKWARA SIMBA, YANGA NA AZAM FC

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.