Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » LAMINE YAMAL KUSALIA BARCA MPAKA 2031, APEWA JEZI YA HESHIMA
    KIMATAIFA

    LAMINE YAMAL KUSALIA BARCA MPAKA 2031, APEWA JEZI YA HESHIMA

    ChikaoBy ChikaoJuly 17, 202502 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    Kinda mahiri wa FC Barcelona, Lamine Yamal, ametia saini mkataba mpya wa muda mrefu na klabu hiyo, ambao utamuweka Camp Nou hadi tarehe 30 Juni 2031. Tangazo hilo lilifanywa rasmi na Barcelona Jumanne, na limeambatana na hatua ya kihistoria ambapo Yamal amekabidhiwa rasmi jezi namba 10, namba yenye heshima kubwa katika historia ya klabu hiyo.

    Jezi hiyo imewahi kuvaliwa na vigogo wa soka kama Ronaldinho Gaucho, Lionel Messi, na hivi karibuni Ansu Fati, na sasa ni zamu ya Yamal kuibeba, ishara ya imani kubwa ya klabu kwake.

    Yamal, ambaye hivi karibuni alitimiza miaka 18, amekuwa gumzo barani Ulaya kutokana na uwezo wake wa kipekee uwanjani. Amevunja rekodi mbalimbali akiwa na umri mdogo katika La Liga, na ameng’ara pia katika mashindano ya kimataifa ikiwemo UEFA Euro 2024, ambapo alionyesha kiwango cha juu licha ya umri wake mdogo.

    Katika hafla ya kusaini mkataba huo, iliyofanyika kwenye ofisi za klabu ya Barcelona, Yamal alisindikizwa na bibi yake mpendwa, huku tukio hilo likihudhuriwa pia na Rais wa klabu Joan Laporta pamoja na Mkurugenzi wa Michezo Deco.

    Mara baada ya kusaini mkataba huo, Yamal alizungumza kwa hisia kali akisema:

    “Barça ni klabu ya maisha yangu. Ndoto yangu imetimia. Nafurahi sana kuona familia yangu hapa leo. Nitapambana kwa ajili ya klabu hii ambayo imenilea.”

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleFADLU DAVIDS ATAJA NI WACHEZAJI GANI WATABAKI SIMBA
    Next Article TETESI ZA USAJILI LIGI KUU YA NBC MSIMU WA 2026/2026

    Related Posts

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    April 17, 2026

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    April 16, 2026

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    April 7, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    SINGIDA BLACK STARS WAZIPIGA MKWARA SIMBA, YANGA NA AZAM FC

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.