Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » OFISA HABARI WA AZAM FC ANALITAKA JIMBO
    KITAIFA

    OFISA HABARI WA AZAM FC ANALITAKA JIMBO

    ChikaoBy ChikaoJune 29, 202501 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    HASHEEM Ibwe, Ofisa Habari wa Klabu ya Azam FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, ametangaza nia ya kuwania ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM)

    Ibwe amesema: “Salamu kwa Vijana wenzangu. Huu ni wakati wa kusimama imara, kuchukua nafasi na kuwa sehemu ya mabadiliko tunayoyataka kuyaona katika jamii zetu. Maendeleo hayaji kwa kusubiri, yanajengwa na watu wenye maono, bidii, na moyo wa kujitolea. Na hakuna kikundi chenye nguvu, maarifa, na ari kubwa kama sisi vijana.

    “Tuna nguvu. Tuna uwezo. Tuna wajibu. Tushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ikiwemo suala la uongozi kuchora dira yetu wenyewe. Kama si sisi, ni nani? Kama si sasa, ni lini?

    “Natangaza rasmi nia yangu thabiti ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM) ya kupeperusha bendera ya  chama jimbo la Mwanga, Kilimanjaro mkoa na wilaya ninayotoka.

    “Tuungane kwa pamoja, tuamke, na tuijenge Tanzania mpya yenye maendeleo ya kweli yanayoanzia kwa vijana.”

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleTFF YATOA MAELEKEZO KWA WAGOMBEA WA UCHAGUZI MKUU 2025
    Next Article MBEBA MIKOBA YA CHAMA KWENYE MTEGO SIMBA SC

    Related Posts

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    April 8, 2026

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    April 8, 2026

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    April 7, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    MBAPPE: NITACHEZEA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.