Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home ยป KISA KUMPIGA MWAMUZI, ‘KIHIMBWA’ ASIMAMISHWA FOUNTAIN GATE FC
    KITAIFA

    KISA KUMPIGA MWAMUZI, ‘KIHIMBWA’ ASIMAMISHWA FOUNTAIN GATE FC

    ChikaoBy ChikaoJune 14, 202502 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Fountain Gate FC
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    Uongozi wa timu ya Fountain Gate FC yenye makazi yake Babati mkoani Manyara imemsimamisha nyota wao Salum Kihimbwa kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu.

    Kihimbwa msimu huu amekuwa na kiwango bora katika Ligi Kuu Bara, ambapo amehusika katika mabao tisa ndani ya timu hiyo, akifunga nne na kutoa pasi za mabao matano.

    Amesimamishwa kwa muda usiojulikana baada ya kumpiga mwamuzi katika mchezo wa kirafiki ambao Fountain Gate ilicheza dhidi ya Wapolo FC katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha.

    Katika mchezo huo wa kirafiki Kihimbwa alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi mchezaji wa Wapolo FC ambapo mchezaji huyo alionekana kupinga maamuzi ya mwamuzi wa kati na kumpiga ngumi ya uso. Wakati huo Fountain Gate ilikuwa inaongoza kwa magoli 2-1.

    Mratibu wa Fountain Gate FC, Wendo Makau ameiambia Mwanaspoti kuwa wamefikia uamuzi wa kumsimamisha mchezo huyo kwa muda usiojulikana ili kulinda taswira ya timu yao ambayo wameijenga muda mrefu.

    “Kwetu sisi kama Fountain Gate mchezaji asipokuwa na nidhamu hata awe na kiwango kizuri vipi tunamtoa kwa hiyo Kihimbwa anaweza kurudi au asirudi,” amesema Makau.

    Ametumia fursa hiyo kuwataka wachezaji wote kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ili kulinda taswira ya timu huku wakitambua kuwa mpira ni ajira na ajira yoyote ile inahitaji nidhamu ya hali ya juu.

    Fountain Gate FC imeweka kambi jijini Arusha kwa ajili ya maandalizi kuelekea mechi mbili za Ligi Kuu Bara ambazo zimesalia kwa upande wao dhidi ya Coastal Union FC na Azam FC ambazo ni muhimu kushinda ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kukwepa kucheza hatua ya mtoano (play off).

    Fountain Gate FC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleTFF YATANGAZA UCHAGUZI MKUU AGOSTI 16, 2025 JIJINI TANGA
    Next Article YANGA SC YAZITAKA TATU ZA TANZANIA PRISONS

    Related Posts

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    April 19, 2026

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    April 19, 2026

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    April 19, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    SINGIDA BLACK STARS WAZIPIGA MKWARA SIMBA, YANGA NA AZAM FC

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.